LONDON, England

MIKEL ARTETA anaamini Arsenal bado wako vizuri kuzikabili  changamoto za kutwaa taji la Ligi Kuu.Arteta aliiongoza Arsenal kumaliza nafasi ya nane katika msimu uliopita na sasa inataka  kumaliza nne bora ili kuirudisha klabu kwenye Ligi ya Mabingwa.

 Washika bunduki waliimarisha safu yao ya kiungo kwenye dirisha la majira ya joto na usajili wa pauni milioni 45 wa Thomas Partey kutoka Atletico Madrid.

Lakini Arteta ana hamu ya Arsenal kujiimarisha zaidi kabla ya kufikiria kufika juu. Alipoulizwa umbali gani Arsenal kutoka kuwa wapinzani wa taji la Ligi Kuu, Arteta aliiambia Sky Sports: ‘Hiyo itachukua michezo michache kufanya hivyo.

‘Lakini ikiwa hauheshimu michakato na unauliza watu fulani wafanye mambo fulani wakati misingi haipo, ni jambo la hatari sana kufanya.

‘Najua sote tunataka kuiona Arsenal iko kileleni mwa ligi. Nia yangu pekee kila wakati ni kuandaa mechi ya mpira wa miguu.

 Bado kuna mambo mengi ambayo yatatokea. ‘Lazima tujiandae kwa wakati mgumu.Tulijua hilo tangu mwanzo kwa sababu sio jambo ambalo limetokea mwaka uliopita – limetokea miaka mingi huko nyuma. ‘Kuibadilisha kuwa ligi na michezo 38, hiyo ni changamoto kubwa. Lakini sote tuko tayari. ‘