PARIS, Ufaransa

ANGEL GOMES amesema aliondoka Manchester United baada ya kukataa ofa yao, na kujiunga na Lille msimu wa joto.

Winga huyo  aliyetokea kituo cha kukuza watoto cha United akiwa na miaka sita, na alianza kucheza timu kubwa mwaka 2017, na kuwa mchezaji mchanga zaidi kuichezea United tangu Duncan Edwards mnamo 1953.

Chini Ole Gunnar Solskjaer msimu ulipita, Gomes alionekena katika michezo sita ya mashindano yote.Na mkataba wake ulimalizika msimu huu, Games alichukua maamuzi ya kuondoka Old Trafford akiwa mchezaji huru kuelekea Lille,

Lille ambayo nayo ilimpeleka kwa mkopo klabu ya Boavista ya Ureno.Katika mazungumzo yake na ‘The Independent’Gomes alisema ‘Ni klabu maalum lakini nilitaka kuweza kucheza na kujielezea’.

‘Nilipewa mkataba mzuri, nilikuwa na familia yangu yote na marafiki karibu nami, lakini niliamua kuwa niko tayari kujitolea ili kufuata njia tofauti.

Ni ngumu kuelewa jinsi uamuzi huo ulikuwa mgumu.Bado ni mshabiki wa United Bado ninaangalia kila mchezo sasa, iwe ni timu ya kwanza au U-18. ‘Ningeweza kukaa na kwenda kwa mkopo lakini nilihisi tu kama ninahitaji mwanzo mpya na nilipitia mambo mengi.

‘Nilikuwa na watu sahihi karibu nami na nilibaki nikiwa na msingi, lakini unapoanguka kidogo huanza kukujenga.

  ‘Inaweza kuwa ngumu kuonyesha hisia zako na lazima uendelee kutoa bidii yako yote kwenye mafunzo.

‘Lakini ukienda nyumbani, chini kabisa unajua wewe sio sawa kabisa na kawaida.’Kwa kawaida mimi ni mpole sana na familia yako hugundua mabadiliko hayo madogo kwako. “Nilitaka kurudi mahali nilipokuwa na kupata furaha katika mpira.”