WAPENZI wasomaji wetu leo hii tunaendelea tena na masaptasapta yetu ambapo nimewandalia chakula mwanana cha Mkate wa kukaanga wenye mayai na mdalasini.

Hivyo ungana name kwa maelekezo ya kuutayarisha upishi huo ikiwa ni pamoja na vipimo na namna ya unavyopikwa.

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 30

MAHITAJI

Kijiko 1 cha chakula unga wa ngano
½ kikombe maziwa
¼ kijiko cha chai chumvi
Mayai 2
¼ kijiko cha chai mdalasini
½ kijiko cha chai vanilla
Kijiko 1 cha chai sukari nyeupe
Mkate vipande 6
Siagi na mafuta kwa ajili ya kukaangia

MAELEKEZO

Kwenye bakuli kubwa, weka maziwa, mayai, chumvi na sukari. ongeza maziwa koroga vizuri. Ongeza vanilla, mdalasini naunga wa ngano . Changanya hadi ilainike vizuri.

Paka mafuta na siagi kiasi kwenye kikaangia katika moto wa wastani. Loweka mkate kwenye mchanganyiko wa unga na mayai hadi ukolee vizuri. Weka mkate kwenye kwenye kikaango.

Pika pande zote mpaka uwe na rangi ya kahawia ila usikauke wala kuungua.Enjoy na ma aple syrup, matunda, asali, ice cream na kingine chochote utakachopenda.