LONDON, England

MENEJA wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema kiungo Bruno Fernandes, amekuwa sehemu muhimu ya timu hiyo siku za hivi karibuni kulinganisha na Cristiano Ronaldo.

Kuwasili kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno mnamo Januari kulileta mabadiliko makubwa ndani ya United katika kipindi cha nusu ya pili ya msimu uliopita na amekuwa katika hali nzuri katika kipindi cha wiki chache zilizopita

Kwa ujumla, Fernandes amefunga mabao 21 katika mechi 35 akiwa na United tangu ajiunge nayo kutoka Sporting Lisbon ya Ureno.

Tunaweza tu kuangalia matokeo tangu ameingia, ana nguvu nyingi, yeye ni mchezaji mzuri ,ni ufunguo hapa sasa kwetu kwenda mbele.

Sikuwa nikitarajia kumwambia Bruno kwamba alikuwa akipumzika dhidi ya Leipzig kwa ushindi wa 5-0 wa Ligi ya Mabingwa mwezi uliopita, lakini haikuwa shida kabisa.

Bruno amethibitisha kwamba, mara kwa mara, kwamba ni timu kabla ya mimi. ‘

Baada ya kufungwa dhidi ya Istanbul Basaksehir na Arsenal, United wamepata ushindi mara tatu mfululizo, lakini wanakabiliwa na kazi ngumu ikiwa kama wanataka kupata nafasi za juu pale watakapokutana na Southampton huko St Mary leo Jumapili .