NA SHARIFFA MAULID,   

WAZIRI Wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi ,Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Ramahan Soraga,  amewataka wafanyakazi     wa Idara ya Maendeleo ya Ushirika, kufanyakazi kwa bidii ili kuhakikisha vyama vya Ushirika vinakua na ustawi  na kudumu zake.

Hayo ameyasema wakati akizungumza na wafanyakazi wa Idara  ya Ushirika, mara baada ya kutembelea vitengo vya taasisi hiyo Migombani Mjini Zanzibar .

Amesema vyama hivyo ndio chanzo cha kujikwamua na umaskini, kwani vimekuwa mategemeo makubwa katika sekta hiyo kuvifanya visimame na kujiendesha.

Hivyo watendaji hao wametakiwa kufahamu kuwa wana mamlaka ya kuwasaidia na kuwaongoza wanaushirika katika kukuza mitaji yao na kuendesha shughuli  zao za Ujasiriamali Kitaalamu.

“Tena Msingi mzuri wa kuona ajira zinapatikana kupitia Ushirika ,Ajira 3,000 zinatakiwa kuzalishwa na waomba washajihisheni Vijana kujiunga nna vikundi hivi linawezekana ”Alisema.

Soraga amesema katika kutembelea Idara hiyo, ameona changamoto mbali mbali na kuahidi kuwa Wizara itatoa ushirikiano kuona watendaji wanafanyakazi kwa ufanisi katika kuviimarisha vikundi hivyo hapa Zanzibar na amewataka kuwa wazalendo kwani serikali ni sikivu.

Nao Maafisa Ushirika wameomba kuunganishwa na Benki ziliopo Tanzania Bara zikiwemo  NMB, TADB ili Wafanyabiashara na Wajasiriamaali  wapatiwe Mikopo na kupatiwa mafunzo ili waweze kutekeleza majukumu yao.