NEW DELHI, INDIA

MAELFU ya wakulima wa India wanaendelea na maandamano ndani na maeneo karibu ya mji mkuu New Delhi, dhidi ya sheria ya kilimo ambayo wanasema inaweza kutumiwa na sekta binafsi kununua mazao yao kwa bei ya chini.

Baada ya mapigano ya siku moja na polisi waliotumia mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na kuwarudisha nyuma, mwishoni wakulima hao waliruhusiwa kuingia New Delhi.

“Tumeita mashirika yote ya wakulima mnamo Disemba 3 na tumezungumza hapo awali na bado tuko tayari kwa mazungumzo,” Tomar alisema.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, hakukuwa na jibu la haraka kutoka kwa viongozi wa maandamano hayo, ambapo waandamanaji walisema hawatarudi nyumbani kwao hadi matakwa yao yatimizwe.

Kwa miezi miwili iliyopita, vyama vya wakulima vilikataa sheria hizo, zilipiga kambi kwenye barabara kuu katika majimbo ya Punjab na Haryana.

Wanasema hatua hiyo inaweza kusababisha serikali kuacha kununua nafaka kwa bei ya uhakika na kusababisha unyonyaji wao kwa mashirika ambayo yangalinunua mazao yao kwa bei rahisi.

Serikali inasema sheria zinahitajika kurekebisha kilimo kwa kuwapa wakulima uhuru wa kuuza mazao yao na kukuza uzalishaji kupitia uwekezaji wa binafsi.