VIENNA,AUSTRIA

AUSTRIA imekiri kwamba kulikuwa na uzembe katika Idara za usalama uliosababisha kutokea shambulizi baya la bunduki mjini Vienna lililofanywa na aliyekuwa mfuasi wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.

Waziri wa Mambo ya ndani wa Austria Karl Nehammer alisema Idara za Ujasusi zilipewa onyo kutoka taifa jirani la Slovakia kuwa mshambuliaji huyo alijaribu kununua risasi lakini zilishindwa kufuatilia kwa karibu.

Mshambuliaji huyo aliyetambuliwa kuwa kijana wa miaka 20 mwenye uraia pacha wa Macedonia na Austria aliuwawa na polisi baada ya kufyetua ovyo bunduki katikati ya mji wa Vienna, katika kisa kilichowauwa watu wanne.

Polisi tayari inawashikilia watu 14 kuhusiana na shambulizi hilo,ambalo ni kubwa kuwahi kutokea nchini Austria katika kipindi cha miongo kadhaa na la kwanza kuhusishwa na mfuasi wa itikadi kali.