NA MARYAM HASSAN

JUMUIYA ya Maendeo ya Vijana na Uhifadhi wa Mazingira iliyopo Bububu (BYDECO), imeipongeza Tume Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kusimamia vyema uchaguzi ulifanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Katibu wa jumuiya hiyo, Zaituni Khairalla Tawakal, wakati akizunguza na Zanzibar leo ofisini kwake Bububu wilaya ya Magharibi ‘A’, Unguja.

Alisema zeozi hilo limefanyika kwa amani licha ya kuwepo kwa baadhi wa wananchi waliotaka kuharibu lakini alivipongeza vyombo vya ulizi la usalama kwa kuwadhibiti.

Alisema tume hiyo imeendesha uchaguzi kwa uwazi na haki na kila ambae ana haki ya kupiga kura aliitumia vyema fursa hiyo.

“Uchaguzi umemalizika salama, sasa tunasubiri mema tuliyoahidiwa na viongozi wetu wakati wa kampeni ili tufaidike nayo,” alisema.

Uchaguzi huo ulishirikisha vyama 17 kwa upande wa Urais wa Zanzibar na vyama 15 katika Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Dk. Hussein Ali Mwinyi na Dk. John Pombe Magufuli wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliibuka washindi katika uchaguzi.