KIGALI,RWANDA

UONGOZI wa chuo kikuu cha KIM nchini Rwanda umetangaza kwamba chuo hakitofunguliwa tena kwa ajili ya masomo na shughuli nyengine kutokana na matatizo ya kifedha.

Aidha Chuo kilitangaza maendeleo yake ambapo kwa mujibu wa maelezo ya Makamu mkuu wa chuo Jean-Baptiste Mugabe alisema maamuzi hayo yalitolewa kufuatia mazungumzo ya pamoja baina ya Uongozi wa chuo na wanafunzi ambao waliwakilishwa  yaliyofanyika Oktoba 20,mwaka huu.

“Ofisi ya Makamu mkuu wa chuo inapenda kuwaarifu wanafunzi wote kwamba kutokana na matatizo ya kifedha chuo hakitofunguliwa kwa ajili ya ufundishaji wala hakutokuwa na shughuli nyengine zozote zitakazoendelea”,taarifa ya Mkuu huyo ilieleza.

Hatua hiyo inakuja ndani ya mwezi mmoja baada ya vyuo vyengine kuanza upya masomo yao baada ya kufungwa kwa takriban miezi minane kwa janga la corona.

Chuo kilishauri wanafunzi kwamba kutafuta njia za kujiunga na taasisi nyengine.