GENEVA ni mji maarufu sana barani Ulaya unaopatikana katika nchi ya Switzerland ama Uswizi, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2017, mji huo una wakaazi 198,979.

Pamoja na kwamba katika mji huo watu wengi wanazungumza lugha ya kifaransa, nchini Uswizi, pia lugha kama kitaliano na kijerumani pia lugha zinazozungumzwa na wananchi wengi wa taifa hilo.

Umaarufu wa jiji la Geneva pia umeongezeka kutokana na Umoja wa Mataifa, taasisi na mashirika mbalimbali ya kimataifa kuweka ofisi zake katika jiji hilo ambalo linaelezwa kuwa na utulivu.

Jiji hilo limekuwa sehemu muhimu ya kibiashara duniani kutokana na makao makuu ya benki nyingi kubwa hapa duniani pamoja na taasisi na mashirika mengine ya kifedha.

Geneva ni mji wenye utajiri mkubwa, ambapo mbali ya kuwepo mabenki ya kimataifa pia katika mji huo kuna majumba ya mnada ya Sotheby na Christie, ambayo huuza mawe yenye thamani.

Hivi karibuni mji huo umechukua hatua kutekeleza kiwango cha juu zaidi cha malipo ya chini ya mshahara wa kila mwezi kujibu wa matakwa ya watu katika kura ya maoni iliyofanyika mnamo mwezi Septemba.

Kiwango kimpya cha malipo ya faranga 23 za Uswizi ambacho ni sawa na euro19, dola 25 ama paundi 22 kitalipwa kwa watu wa kiwango cha chini zaidi cha mshahara kuwa euro 3,350.

Mji huo wa Uswizi huenda ukawa na utajiri mkubwa lakini pia ni nyumbani kwa maelfu ya wafanyakazi wa hoteli, wahudumu wa migahawa, watu wanaotoa huduma za usafi na wafanyakazi wa saluni ambao wanajitahidi kumudu ghara ya juu ya maisha.

Wakati Switzerland ilipoweka amri ya kutotoka nje mwezi Machi mwaka 20202 ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona, picha za milolongo mirefu ya watu waliokuwa wakisubiri kupokea msaada wa chakula mjini Geneva ziligongwa vichwa vya habari.

Mpango huo wa chakula ulikuwepo hata kabla ya janga la corona na bado upo hata baada ya sheria yakutotoka nje kuondolewa miezi kadhaa iliyopita baada ya kupungua kwa maambukizi ua virusi vya corona.

Charly Hernandez mshirikishi katika shirika la msaada Colis du Coeur ambalo linagawanya maelfu ya bidhaa za chakula kila wiki katika maeneo ya kati ya mji huo alisema kwamba wanawake wengi ndio wanaopanga foleni wakiwa na watoto wao kupokea chakula.

“Chumba kimoja kinakodishwa kwa faranga 1,000 kwa mwezi, ikiwa utafanikiwa kununua chakula kwa faranga 500 kwa mwezi basi wewe ni hodari kwa kubana matumizi, bima ya afya ni 550 kwa mwezi kwa kila mtu. Ukiwa na mke na watoto wawili niambie utasalia na nini?’, alisema.

Sheria hiyo mpya ya malipo inachoweka kiwango cha chini cha mshahara itawasaidia watu wengi, ambao wamekuwa wakila vyakula vya bei nafuu migahawani.

Hata baadhi ya watu wanaojitolea kufanya kazi, wanahisi gharama za maisha mjini Geneva ziko juu sana, huku wananchi wenye kipato cha chini kushindwa hata kupata nyumba nzuri ya kuishi.

Biashara zinazowalipa wafanyakazi chini ya faranga 23 kwa saa watalazimika kuwaongezea malipo. Hatua ya kutekeleza malipo hayo mapya kati kati ya janga la corona ambalo limechangia kushuka kwa faida itakuwa na athari kubwa.

Mmoja wa wamiliki wa migahawa, Stefano Fanari, wameambia kituo cha televisheni cha Uswizi kwamba haoni ikiwa atamudu kulipa ada inayotakiwa. Kama mpishi mkuu, marupurupu yake ya mwezi ni kati ya faranga 5,000 na 6,000 kwa mwezi.

“Nitawezaje kuendelea wakati natakiwa kuwalipa waosha vyombo kiasi hicho cha fedha?

“Je nipunguze saa zao za kufanya kazi? Msinielewe vibaya, Sipingi suala la wao kulipwa 4,000 kwa mwezi. Lakini kwa hali ilivyo hatuwezi kumudu malipo hayo. Nimejitolea, Nafanya kazi hapa kwa saa 12 kwa siku. Nifanye nini?”

Mshahara wa chini wa Geneva umeidhinishwa kuwa sheria sio kwa sababu ni hatua iliyowekwa na serikali, bali ni kutokana na pendekezo la wananchi mjini huo.

Walikusanya saini nyingi kutaka suala hilo lipigiwe kura ya maoni na kufikia Septemba 27 mwaka 2020 wapiga kura waliitikia ndio, kwa kwa asilimia 58 dhidi ya asilimia 42.

Mfumo wa Uswizi wa demokrasia ya moja kwa moja unamaanisha kwamba wapiga kura wanauamuzi wa mwisho, kiwango cha chini cha mshahara sasa ni wa chini ni lazima.

Mara nyingi, raia wa Uswizi hupiga kura kwa makini sana linapokuja suala la matumizi ya fedha za umma. Lakini siku hiyo hiyo pia waliunga mkono likizo ya wiki mbili ya uzazi kwa mzazi wa kiume ambayo italipwa.

Kwa Charly Hernandez hatua hizi ni dalili njema, hususan nyakati hizi ngumu. “Walipigia kura, na hilo limenifurahisha sana. Tuna demokrasia ya moja kwa moja na hilo ni jambp zurisana, lakini kile watu wasichokijua ni kwamba juhudi nyingi za kiraia hupuuzwa.

“Ni vyema kwamba mambo yameanza kubadilika na baadhi ya vitu vinaidhinishwa na kwa hivyo naamini mambo yanazidi kuimarika … Japo kwa mwendo wa pole pole, lakini ndio kasi ya Uswizi.”

Mtihani mwingine kwa wapiga kura utakuja baadaye mwezi huu wakati raia wa Uswizi wataamua kuhusu mpango wa uwajibikaji wa biashara.

Mpango huo utazihitaji kampuni zilizo na makao yake Switzerland kuwajibikia kisheria na kifedha ukiukwaji wa haki za kibinadamu katika hatua zote za utendaji wa kampuni hizo mahali popote duniani.

Kura ya ndio kwa pendkezo hilo huenda ikagharimu zaidi ya mshahara ya chini wa Geneva.