NA ZAINAB ATUPAE

KOCHA mkuu wa timu ya Gulioni City Mahad Mussa Haji, amesema wakati wowote anataraji kuanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na ligi daraja la pili Mkoa wa Mjini.

Mahad aliyasema hayo hivi karibuni huko Kikwajuni wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa gazeti hili.

Alisema walikuwa wanasubiri uchaguzi mkuu ambao tayari umemalizika,hivyo aliwaka wachezaji,mashabiki pamoja na viongozi kukaa tayari juu ya hilo.

Akizungumzia  usajili,alisema msimu huu alifanya usajili mdogo kwani wachezaji alikuwa nao wote ni wazuri ambao wana uwezo wa kuibebea timu hiyo.

Alisema aliongeza wachezaji watano na kuwaacha wanne ambao wamejiunga na timu tofauti.

Hata hivyo alisema anatarajia kuwatangaza wachezaji hao siku ambayo wataanza mazoezi kwenye uwanja wa Mbuyuni uliopo Malindi.

Aidha alisema msimu huu wana malengo mengi,ikiwemo kuipandisha timu daraja kutoka la pili Mkoa kwenda la kwanza kanda ya Unguja.

Alisema watahakikisha wanapambana kwa kila hali ili  kupata  nafasi ya kupanda daraja.