BAGHDAD,IRAQ

RAIS  wa Irag ameridhia sheria mpya ya uchagzuzi ambayo itatoa ruhusa kwa wagombea huru kushinda nafasi za ubunge, ikiwa hatua ya kuweka mambo sawa kuelekea uchaguzi wa mapema mwakani.

Rais Barham Saleh alisisitiza uhitaji wa uchaguzi huru,wa haki na uwazi katika zoezi la kuhesabu kura kwa lengo la kuwajengea imani wananchi wa taifa hilo katika mchakato mzima wa uchaguzi.

Sheria mpya ilibadili majimbo 18 ya uchaguzi ambayo yalikuwa yakitumika awali, kuwa wilaya na kuvizuia vyama kushiriki pasipo na upinzani katika maeneo hayo ambapo ilivisaidia kujinyakulia viti vyote vya ubunge katika baadhi ya maeneo.

Kwa hivyo sasa kura anaweza kupigiwa yoyote mshiriki katika kinyang’anyiro cha wilaya.

Mabadiliko hayo ni muhimu kwa kuleta utulivu nchini Iraq na hasa Baghdad, ambayo ilikumbwa na maandamano mwaka uliopita.