WAGADURU,BURKINA FASO

RAIS wa Burkina Faso Roch Marc Chrstian Kabore, amezindua kampeni yake ya kugombea muhula mwengine madarakani, akiahidi kuimarisha usalama na amani nchini humo.

Burkina Faso imekuwa ikikumbwa na mashambulizi kutoka makundi ya wapiganaji kwa muda wa miaka mitano sasa.

Akihutubia wafuasi wake zaidi ya 25,000 mjini Bobo Dioulasso, Kabore aliahidi kwamba ataendelea kupigana na makundi hayo ya wapiganaji hadi amani itakapopatikana nchini humo.

Anagombea muhula wa pili madarakani na alisema lengo lake kubwa ni usalama wa nchi hiyo.

Roch Marc Christian, anakabiliwa na ushindani kutoka kwa wagombea wengine 12 katika uchaguzi huo wa Novemba 22.