LONDON, England

NYOTA wa klabu ya Tottenham Hotspur Harry Kane ameweka rekodi ya kufikisha jumla ya mabao 200 klabuni hapo.

Kane alifikisha idadi hiyo baada ya kufunga bao  kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ludogorets kwenye Ligi ya Europa, Novemba 5.

Anakuwa ni mchezaji wa tatu kufikisha idadi ya mabao hayo ndani ya Spurs akiwa nyuma ya Bobby Smith, mwenye mabao 208 na Jimmy Greaves mwenye mabao 266.

Kane ametupia jumla ya mabao 12 kwenye michuano yote na ametoa pasi za kufunga 10.