NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewatangazia wananchi kwamba Jumatatu ya Novemba 2 mwaka huu itakuwa siku ya mapumziko.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk. Shein ameifanya siku hiyo iwe ya mapumziko ili kutoa nafasi kwa watumishi wa umma na wananchi wahudhurie kuapishwa kwa rais mteule, Dk. Hussein Mwinyi.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba Dk. Shein ametangaza siku hiyo kuwa mapumziko kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 6(1)(a) cha sheria ya mambo ya Rais nambari 3 ya mwaka 2020”, ilieleza taarifa hiyo.