LONDON, England

MANCHESTER UNITED wamefanya mazungumzo na Mauricio Pochettino ili kuchukua nafasi ya kocha aliyopo sasa Ole Gunnar Solskjaer.

Solskjaer yupo kwenye presha kubwa ya kibarua chake kuota nyasi kufuatia matokeo mabaya ya dhidi ya Arsenal kwenye ligi kuu na  yale ya Istanbul Basaksehir katika lii ya mabingwa,  hivyo kujikuta akiingia kwenye kitabu cha wanaotarajiwa kutimuliwa.

Kwa mujibu wa Manchester Evening News, United wamewasiliana na Pochettino kuchukua mikoba.

Hata hivyo inadaiwa hapo awali Pochettino amewahi kutamani kuifundisha United, hivyo wanaamini kocha huyo bado hajabadili maamuzi yake.