VIENNA,AUSTRIA

MSHAMBULIAJI aliyehusika na shambulizi la bunduki mjini Vienna lililosababisha vifo vya watu wanne alikuwa mfuasi wa kundi linalojiita Dola la Kiislam, IS.

Hayo yalielezwa na Serikali ya Austria ambayo ilisema kijana huyo Kujtim Fejzulai aliyekuwa na umri wa miaka 20, alitiwa hatiani mwaka uliopita kwa kujaribu kusafiri kwenda Syria kwa lengo la kujiunga na kundi la IS.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya ndani ya Austria, Fejzulai, ambaye alikuwa na uraia pacha wa Macedonia na Austria alihukumiwa miezi 22 jena lakini alitolewa kwa msahama chini ya utaratibu wa kurekebisha tabia .

Disemba iliyopita Fejzulai aliuwawa na polisi muda mfupi baada ya kutekeleza shambulizi hilo na alikutwa akiwa na bunduki ya rashasha, bastola na mkanda bandia wa mabomu.

Katika tukio hilo washambuliaji kadhaa ikiwemo Fejzulai walifyetua risasi katikati ya mji Vienna na kusababisha vifo, majeruhi na taharuki kubwa.