YAMOUSSOUKRO,IVORY COAST

RAIS Alassane Ouattara ameibuka mshindi katika uchaguzi wa rais nchini Ivory Coast huku wapinzani walioususia uchaguzi huo wakisema wataunda Serikali ya mpito.

Tume huru ya Uchaguzi (CEI) ilitangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais uliofanyika,Oktoba 31 ambapo Ouattara aliibuka mshindi kwa 94.27% ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

Henri Konan Bédié alipata asilimia 1.66, Kouadio Konan Bertin alipata asilimia 1.99 na Pascal Affi N’guessan alipata asilimia 0.99% ya kura zilizopigwa.

Tume hiyo ilisema kiwango cha ushiriki kulingana na IEC ni 53.90%. Matokeo haya yanatarajiwa kuthibitishwa na Mahakama ya Katiba.

Wapinzani Ivory Coast ambao walisusia uchaguzi wa urais,walisema wataunda serikali ya mpito.

Rais Ouattara, 78,amekuwa madarakani kwa takriban muongo mzima, lakini anadai katiba mpya iliyoidhinishwa mwaka 2016 inamruhusu kugombea tena urais kwa muhula wa tatu.