NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

ALIYEWAHI kuwa nahodha wa klabu ya Yanga, Pappy Tshishimbi, amesema kuwa hana mpango wa kujiunga na Simba kwa sasa.

Tshishimbi raia wa DRC Congo aliachana na Wanajangwani hao msimu huu na kujiunga na kikosi cha AS Vita  cha nchini kwao.

Kiungo huyo tangu akiwa Yanga hadi hivi sasa amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba.

Akizungumza na Zanzibar Leo kwa njia ya mtandao, Tshishimbi, amesema hata kama Simba wanamtaka lakini  katika kichwa chake bado hajaweka nia hiyo.

Alisema anacho kifikiria kwa wakati huu ni kuisadia timu yake kupata mafanikio.

“Mimi kwa sasa akilini kwangu hakuna Simba wala Yanga, kama wao wananihitaji mimi siwezi kusema lolote, maana sina ninachofahamu lakini sifikirii hayo,” alisema

Tshishimbi aliachana na Yanga baada ya mkataba wake kumalizika.