Tyrese Campbell
KLABU za Rangers na Celtic zilifanya mazungumzo ya kumsaini, Tyrese Campbell kabla ya mshambuliaji huyo kushawishika kusaini nyongeza ya mkataba huko Stoke.
Baba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, nyota wa zamani wa Arsenal, Kevin Campbell, mazungumzo yalifanywa na vigogo hivyo.(Goal).

Lautaro Martinez
KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane, angelipendelea kumsaini, Lautaro Martinez kutoka Inter kuliko nyota wa Borussia Dortmund, Erling Haaland.
Zidane anaamini Lautaro atafaa kwa mtindo wake wa kucheza vizuri. (Goal).

Nigel Pearson
KOCHA wa zamani wa Watford, Nigel Pearson, amesema wachezaji wake walijua alikuwa akikatwa kwa shoka kabla ya kuambiwa na klabu.
Pearson alifukuzwa na Hornets michezo miwili kabla ya kumalizika kwa msimu uliopita, wakati klabu ikiondolewa kutoka Ligi Kuu ya England.(Mirror).

Andre-Pierre Gignac
MSHAMBULIAJI, Andre-Pierre Gignac ameahidi uaminifu wake kwa Tigres na amesema hana mpango wa kuondoka klabuni.
“Nimekuwa hapa miaka mitano na natumai ni miaka mengine mitano, hadi nitakapokuwa na miaka 40.”(Telefoot).

Dominik Szoboszlai
KIUNGO, Dominik Szoboszlai ni mlengwa mkubwa wa uhamisho kwa meneja wa Arsenal, Mikel Arteta, mnamo.
Nyota huyo wa Red Bull Salzburg, amekuwa akifuatiliwa kiwango chake na washika bunduki wanaweza kumuangalia kama mbadala wa Houssem Aouar. (Index).

Slaven Bilic
MENEJA wa West Brom, Slaven Bilic, anakaribia kupoteza kibarua chake.
Mcroatia huyo hana furaha na bodi juu ya sera yao ya uhamisho, wakati matokeo mabaya yanafanya timu iwe na shida kubwa kwenye Ligi Kuu ya England.( Daily Mail).

Brahim Diaz
AC Milan wamejiandaa kufanya kila wawezalo kupata mustakabali wa Brahim Diaz.
Baada ya kushindwa kupata kifungu cha ununuzi katika mpango wake wa mkopo, wako tayari kufungua mazungumzo na Real Madrid juu ya uhamisho.(Calciomercato).

Antonio Conte
KOCHA, Antonio Conte anajiandaa kuivamia klabu yake ya zamani ya Chelsea ili kuimarisha kikosi chake cha Inter.
Kocha huyo anataka kumuongeza Olivier Giroud, Emerson Palmieri na Marcos Alonso kwenye safu yake.(Goal).

Junior Firpo
KLABU ya Barcelona ipo tayari kuuza wachezaji watano mnamo Januari.
Martin Braithwaite, Carles Alena, Ousmane Dembele, Junior Firpo na Samuel Umtiti si sehemu ya mipango ya Ronald Koeman na wanajiandaa kuondoka klabu hapo ili kuongezea mfuko wanaouhitaji.(Mundo Deportivo).

Renato Sanches
KIUNGO wa Lille, Renato Sanches, anasakwa na kundi la klabu za Italia.
Baada ya kuvutia kwenye ushindi wa LOSC wa mabao 3-0 dhidi ya AC Milan, Juventus wamevutiwa na kiungo huyo sawa na Milan, Inter, Napoli na Roma.(Calciomercato)