Ibrahima Konate
KLABU ya Arsenal ina azma ya kumsajili beki wa RB Leipzig na Ufaransa, Ibrahima Konate (21), na kiungo wa Ufaransa, Christopher Nkunku (22). (Bild).

Neymar
JUVENTUS ipo tayari kubadilishana wachezaji ambapo mpango huo utamfanya winga, Christiano Ronaldo kujiunga na PSG huku mshambuliaji wa Brazil, Neymar akielekea Juventus. (Tuttomercato).

Lionel Messi
BABA yake Lionel Messi ambaye pia ni wakala wake amekana ripoti kwamba mshambuliaji huyo ana mipango ya kujiunga na PSG kutoka Barcelona msimu. (Goal).

Paul Pogba
MANCHESTER United inapanga kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa, Paul Pogba (27) wakati wa dirisha la uhamisho la msimu ujao. (Talksport).

Son Heung -min
KLABU ya Tottenham Hotspurs imeanza mazungumzo na mshambuliaji wa Korea Kusini, Son Heung -min. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 huenda akapatiwa mkataba hadi 2026 wenye thamani ya pauni 200,000 kwa wiki. (Guardian).

Georginio Wijnaldum
KIUNGO wa Liverpool, Georginio Wijnaldum (30), bado hajatia saini kandarasi mpya. Mkataba wa raia huyo wa Uholanzi katika klabu hiyo unakamilika mwisho wa msimu huu. (Liverpool Echo).

Ronaldo Koeman
MENEJA wa Barcelona, Ronald Koeman, amesema, Wijnaldum huenda akahitajika katika siku zijazo na mabingwa hao wa Hispania. (Sport).

David Alaba
LIVERPOOL imehusishwa na uhamisho wa beki wa Austria, David Alaba, lakini, Bayern Munich haitamuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 mwezi Januari, licha ya mkataba wake kukamilika msimu huu. (Bild).

James Tarkowski
BEKI wa Burnley, James Tarkowski, amesema, ofa ya mkataba mpya sio nzuri ya haja . Mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 27, hana azma ya kuweka mkataba mpya na Clarets. (Telegraph – subscription required)

Mauricio Pochettino
KLABU ya Athletic Bilbao inafikiria kumsajii aliyekuwa meneja wa Tottenham, Muaricio Pochettino kama meneja wao. (Marca).

Fabio Baptista
KLABU za Crystal Palace na Aston Villa zina azma ya kumsajili winga wa Benfica na Ureno, Fabio Baptista (19). (Calciomercato).