MADRID, Hispania

KLABU ya Valencia imewashangaza wengi baada ya kuwachapa Real Madrid mabao 4-1, huku Carlos Soler akifunga mabao matatu (hat-trick) kwa njia ya penalti.

Ajabu ni kuwa Madrid ndio walikuwa wa kwanza kutingisha nyavu za Valencia kupitia na Karim Benzema.

Valencia walisawazisha na baadaye kuendelea na mabao  mengine matatu zaidi.

Soler ameleta kilio hicho kwa Madrid, si siku nyingi baada ya kuaibishwa na klabu ya Ukraine walipochapwa 3-2.

Hiki ni kipigo kikubwa cha pili kwa Real katika msimu huu, na kizito zaidi cha ligi tangu walipofungwa 5-1 na Barcelona mnamo Oktoba 2018.

Madrid wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo kwa pointi 16 baada ya michezo minane, wakati Real Sociedad wakiwa kileleni na pointi 20 baada ya michezo tisa.