HABIBA ZARALI ,PEMBA

WANANCHI Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba wameshauriwa kuzidisha usafi katika maeneo yao yanayowazunguka, ili kuweza kuepuka kujitokeza maradhi ya mripuko yakiwemo matumbo ya kuharisha.

Ushauri huo umetolewa kwa nyakati tofauti na wananchi wilayani humo, walipokuwa wakizungumza na mwandishi wa habari mara baada ya kujitokeza mvua katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Wananchi hao walisema ni vyema kila mmoja kuchukuwa tahadhari za kudumisha usafi kwa makusudi, ili kuepukana na maradhi hayo hatari ambayo kuwepo kwake yanaweza kupoteza maisha ya watu.

Juma Saidi Mkaazi wa Makombeni alisema maradhi ya kuharisha yanapoingia hayachagui mkubwa wala mdogo, hivyo ni vyema kuwa makini katika harakati za maisha yao kwa kuzingatia usafi.

Alisema kwa wananchi wenye akili timamu si vizuri kusubiria kujitokeza tatizo na kuanza kulaumu viongozi ama Serikali na badala yake ni vyema kuchukuwa tahadhari mapema, ili kuepusha tatizo hilo kujitokeza.

“kuna baadhi ya watu hawana tahadhari ya jambo isipokuwa husubiria mpaka tatizo liwepo apo tena ndio ukaona wanatupia lawama upande mmoja jambo ambalo sio sahihi”,alisema.

Akigusia kuhusu wafanyabiashara wa vyakula Fatma bakar Mohamed mkaazi wa Mkoani alisema ni vyema wakachukuwa tahadhari ya kufunika vizuri, ili kuepusha wadudu wanaoweza kueneza maradhi hayo.

Alisema afya za wananchi ni muhimu zaidi kwani yanapotokea machafuko ya kiafya huleta hasara kubwa kwa wananchi na Serikali kwa ujumla ikiwemo kutumia madawa nje ya utaratibu uliokusudiwa.

“Ingawa tunaona wafanyabiashara wengi wanafunika vyakula vyao lakini tahadhari inahitaji kuzidishwa, ili tuweze kuwa na afya