TOKYO,JAPANI

WAPIGA kura katika mji wa magharibi mwa Japani wa Osaka wamepiga kura na kukataa mpango wa kupanga upya mji huo katika kata nne maalumu jijini Tokyo.

Kura zote zikiwa zimehesabiwa, wapiga kura 692,996 walikataa mpango huo wakati 675,829 wakiukubali.

Wanaoupinga walishinda kura ya maoni ya pili kuhusiana na suala hilo, na kuruhusu mfumo wa sasa kuendelea kutumika.

Kinachojulikana kama mpango wa jiji la Osaka ulitaka kuondolewa kwa mji huo ulioundwa kisheria na kuunda kata nne maalumu kuanzia Januari mosi mwaka 2025.

Zaidi ya wapiga kura milioni 2.2 mjini humo walikidhi vigezo vya kushiriki kura hiyo.

Meya wa mji wa Osaka Matsui Ichiro anayeongoza chama cha Osaka Ishin no Kai, aliwaambia wanahabari kuwa atastaafu siasa baada ya kumaliza muhula wake kama meya mwezi Aprili mwaka 2023.

Naye Gavana wa mkoa wa Osaka Yoshimura Hirofumi anayehudumu kama naibu kiongozi wa chama hicho aliwaambia wanahabari kwamba anachukulia kwa uzito kukataliwa huko kwa kura ya maoni.

Alisema hatopendekeza tena mpango wa jiji na anataka kumalizia miaka miwili na nusu iliyobakia ya muhula wake.