LONDON,UINGEREZA

MATAIFA kadhaa ya Umoja wa Ulaya yamekuwa yakipiga marufuku kuingia kwa ndege za abiria zinazotokea nchini Uingereza, ili kuzuia kuenea kwa aina mpya ya virusi vya corona vilivyogunduliwa nchini humo.

Ujerumani pamoja na mataifa mengine kadhaa, yalichukua hatua hiyo baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kutangaza kuzuka kwa aina hiyo mpya ya virusi vya corona kusini mwa Uingereza.

Johnson haraka alitangaza masharti magumu na kuwataka mamilioni ya wanachi wa eneo hilo kubakia majumbani, kwa sababu virusi hivyo vilianza kusambaa kwa kasi kubwa.

Wakati huo huo, Shirika la Dawa la Ulaya, limekutana kuidhinisha chanjo ya kwanza dhidi ya COVID-19 kwa mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya.

Chanjo hiyo itatolewa kwa mamilioni ya raia wa umoja huo.