NA MWANAJUMA MMANGA
WATU wawili wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa baada ya ajali zilizotokea Koani na Bwejuu Wilaya ya Kati na Kusini Unguja.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Unguja, Suleiman Hassan Suleiman, akithibitisha kutokea kwa matukio hayo, aliwataja marehemu hao Mohamed Juma Khatib (25) mkaazi Mwera na Ali Mussa Ali (45) mkaazi wa Bwejuu.
Kamanda Suleiman alisema tukio la kwanza limetokea mnamo siku ya Jumanne Disemba 22, mwaka huu, majira ya saa 12:00 usiku huko Koani.
Alisema kijana Talib Uledi Shaaban (27)askari wa JWTZ wa kambi ya Ubago aliekuwa dereva wa gari namba Z372 JE aina ya IST akitokea Kidimni na kuelekea Mwera.
Alisema kijana huyo, alimgonga mpanda vespa namba Z.770GG aitwae Ali Haji Silima (23) mkaazi wa Magogoni aliyekuwa amempakia Mohamed Juma Khatib, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja na Talib uledi Shaaba amelazwa hospitali ya jeshi Bububu.
Suleiman alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa vespa bila ya kuwasha taa, na kusabaisha vyombo vyote vimepata hasara kubwa.
Tukio la pili limetokea Disemba 25 mwaka huu majira ya saa 4:20 ajali ya kwanza ilimuhusisha tukio hilo limetokea majira ya saa 4:40 usiku huko Bwejuu kwa Lila Wilaya ya kusini Unguja.
Alisema maeneo ya kwa Lila pikipiki namba Z.316 JM aina ya Sound rangi nyekundu iliyokuwa na Enock Narekwa Edale (28) mkaazi wa Bwejuu .
Alisema kijana huyo, alikuwa akitokea Paje na kuelekea Michanvi aligongana uso kwa uso na wapanda vespa namba Z.307 AG aina ya Star rangi nyeusi iliyokuwa ikiendeshwa na Ali Mussa Ali (42) mkaazi wa Bwejuu, akitokea Michanvi na kuelekea Paje, akiwa amepakia Shauri Ahmada Sudi (70) mkaazi wa Bwejuu.
Suleiman alisema katika ajali hiyo, Ali Mussa Ali, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Makunduchi na Shauri Ahmada Sudi na Enock Narekwa wameumia sehemu mbali mbali na wamelazwa katika hospitali ya Makunduchi na hali zao zinaendelea vizuri na vyombo vyote vimepata hasara kubwa.
Hivyo Kamanda Suleiman aliwataka madereva kuwa waaangalifu pale wanapokuwa njiani ili kuepuka jail zisizokuwa za ulazima.