LONDON, England
KLABU ya Arsenal inamfukuzia kiungo wa Sevilla, Joan Jordan, ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kinachosua sua kwenye Ligi Kuu ya England.

Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta, anatajwa kuitazama kwa ukaribu saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Hispania mwezi Januari.

Ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Chelsea kwenye ‘dabi ya London’, umemfanya Arteta afikirie kuongeza nguvu eneo la kiungo ili kupata ushindi zaidi kwenye mechi zake.

Arteta ana matumaini kwamba akipata saini ya nyota huyo ataongeza nguvu ya kujiamini kwa kikosi chake kwa kuwa ana uwezo pia wa kufunga akiwa amecheza mechi 41, amefunga magoli mawili kwenye La Liga’. Arsenal ipo tayari kuweka dau la pauni milioni 32 ili kumpata nyota huyo ambaye amewahi kuichezea Eibar msimu wa 2017-19 na alicheza mechi 71 na kufunga mabao 10.(Goal).