NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa klabu ya Azam FC, umefanikiwa kushusha mshambuliaji wa kimataifa Mpiana Mzonzi raia wa Congo.


Mchezaji huyo ameingia nchini juzi na jana aliendelea na ratiba za vipimo ili kuangalia utimamu wake kabla ya kumwaga wino.


Mzonzi kabla ya kutua Azam alikuwa akiitumikia Lupopo FC ambayo pia aliwahi kucheza Heritier Makambo ambaye amewahi kupita Yanga.


Mchezaji huyo ni sehemu ya kuimarisha katika kipindi hiki cha usajili dirisha dogo.
Akizungumza na Zanzibar Leo jana,Msemaji wa klabu hiyo Zakaria Thabit, alisema wameshusha kifaa kipya ambacho leo(jana) wanakifanyia vipimo na kama atakuwa sawa watampa mkataba wa mwaka mmoja kukitumikia kikosi chao.


Alisema mchezaji huyo ni mbadala wa wachezaji wao wawili ambao wamewauza Iddi Chilunda na Thiery Akono ambaye naye ameuzwa hivi karibuni.