NA ZAINAB ATUPAE
KATIKA kujiandaa na mashindano ya Mawizara,Mashirikana na Taasisi za Serikali timu ya soka ya Bandari leo itashuka uwanjani kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Veterani ya Sayari.


Akizungumza na gazeti hili huko uwanja wa KMKM Maisara msemaji wa timu hiyo Abdulhamid Khamis Baiya,alisema mechi itapigwa katika uwanja wa KMKM Maisara majira ya saa 10:00 jioni.


Alisema mechi hiyo ni miongoni mwa maandalizi ya mashindano hayo ambayo yanatarajia kutimua vumbi mwisho mwa mwezi huu ama mwanzoni mwa Januari 2021.


Alisema timu yao iko vizuri kwani walimaliza mashindano mwezi huu hivyo hawana wasi wasi.
Alisema endapo kamati itakuwa na uadilifu katika mashindano yao wanaimani kubwa kuwa timu yao itafanya vyema.


“Timu yetu ipo vizuri na wachezaji wetu wameajiriwa na hatunamamluki,kama hakutaingizwa mamluki basi tutachukuwa ubingwa,”alisema.


Aidha alisema kwa upande wa mechi hiyo ya kirafiki ambayo watacheza leo watahakikisha wanaondoka na ushindi bila ya wasi wasi