MADRID, Hispania

KARIM Benzema nyota wa kikosi cha Real Madrid amesema kuwa atazidi kupambana ndani ya uwanja ili kufikia mafanikio ambayo anayahitaji.

Ndani ya La Liga, Benzema ni miongoni mwa washambuliaji   watatu wa kutupia nyavuni huku akimpoteza nyota wa Barcelona, Lionel Messi.

Benzema akiwa amecheza mechi 13 ametupia jumla ya mabao manane na pasi tano za mabao huku akiwa amepiga jumla ya mashuti 33.

Wengine wenye mabao manane  ni Iago Aspas wa Celta Vigo na ana pasi tano pia za mabao akiwa amecheza mechi 15 na Gerard Moreno wa Villarreal ametoa pasi moja ya bao na amecheza mechi 13.

Luis Suarez wa Atletico Madrid ametupia mabao saba akiwa amecheza mechi 10 huku Messi wa Barcelona akiwa ametupia mabao saba na pasi moja ya bao kwenye mechi 14.

Benzema ambaye amekuwa haimbwi sana licha ya jitihada zake ndani ya uwanja amesema:”Nitazidi kupambana daima, nina amini kwamba mafanikio hayawezi kuja ikiwa nitashindwa kuongeza juhudi” .