NA VICTORIA GODFREY

UONGOZI wa Chama cha Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es Salaam (DABA) umesema utatumia mfumo wa ligi kwenye mashindano ya ubingwa wa wazi mwaka ujao.

Akizungumza na Gazeti hili,Mwenyekiti wa DABA,Godfrey Akalory,alisema lengo ni kutoa fursa kwa mabondia kucheza mapambano mengi ili kuonyesha vipaji vyao.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuibua na kuendeleza vipaji vilivyopo na vipya, ambavyo vitatumika kwa sasa na baadaye kwenye timu za Taifa.

Wakati huo huo, Kamati ya utendaji wa chama hicho inatarajia kukutana kesho kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo kupitia taarifa ya mwaka mzima.