NA ZAINAB ATUPAE
TIMU ya soka ya Daily Foro imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuichapa mabao 2-0 Real Used, ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya Mbunge wa Malindi Ndondo cup hatua ya robo fainali.


Mchezo huo uliotimua vumbi uwanja wa Mchangani majira ya saa 10: jioni.


Mabao yalifungwa na Ahmed Zahor dakika ya nne na Nadeem Amigo dakika ya 73.


Mchezo uliopigwa uwanja wa Malindi majira ya saa 10: jioni timu ya timu ya Mwembetanga imeungana na Daily Foro kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuichapa kwa penalti 4-3 timu ya Napol FC.


Hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika hakuna timu iliofanikiwa kuliona lango la mwenzake ndipo sheria ya kupiga mikwaju ya penalti ikatumika ili kupata mshindi.


Kwa matokeo hayo timu ya Mwembetanga ilitangulia kuingia hatua ya nusu fainali,huku timu ya Napol FC ikiaga mashindano msimu huu.