NA HAFSA GOLO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali MWinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika fainali ya kombe la Mapinduzi January 13 mwaka 2021.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Dk. Khalid Salum Mohamed, alieleza hayo alipokua akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.

Alisema fainali hiyo itachezwa usiku katika Uwanja wa Amaan.

Dk. Khalid alisema mashindano hayo yataanza Januari 5 mwaka 2021.