NA MWAJUMA JUMA
KOCHA wa timu ya soka ya Dula Boys Abdalla Mwinyi Juma ‘Dula Boys’, amesema sababu kubwa iliyopelekea kufungwa ni wachezaji kutofanya mazoezi ya kutosha ya kujiandaa na ligi hiyo ambayo ilianza wiki iliyopita.


Dula boys ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza Kanda ya Unguja ilishuka dimbani juzi kucheza na Gulioni, ambapo ilifungwa mabao 3 – 0 mchezo uliochezwa uwanja wa Amaan.


Hivyo alisema baada ya kupoteza mchezo huo lakini wataendelea kujipanga ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo inayofuata.


Alisema msimu huu mechi za ligi hiyo zinachezwa nyumbani na ugenini watahakikisha wanafanya vyema hasa zile za nyumbani.


Dula Boys kesho inatarajiwa kushuka dimbani tena kucheza na Kilimani City mchezo ambao utachezwa uwanja wa Mao Zedong.


Mchezo huo unatajwa kuwa na ushindani mkali kwani timu zote zinashuka dimbani zikiwa na machungu ya kufungwa katika michezo yao iliyopita, ambapo Kilimani City walifungwa na New King mabao 2-1 na Dula Boys wakafungwa na Gulioni FC mabao 3-0.