ZURICH, Uswisi
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limetangaza kufutilia mbali michuano ya Kombe la Dunia la Vijana wa chini ya umri wa miaka 17 na 20 kwa wanaume ya mwaka ujao kutokana na janga la ‘corona’.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na FIFA, michuano hiyo iliyopangwa kufanyika mwaka 2021, yamefutwa kwa sababu ya vizuizi vya safari za kimataifa kutokana na janga la ‘corona’, na yatarejea hali ya maisha itakapokuwa ya kawaida.

Taarifa zaidi zilielezea kwamba nchi za Peru na Indonesia, pia zitaweza kulinda haki zao za kuandaa mashindano hayo yatakayofanyika mwaka 2023. Kufuatia uamuzi huu, Peru itakuwa mwenyeji wa maandalizi ya Kombe la Dunia la Vijana wa chini ya miaka 17 na Indonesia itakuwa mwenyeji wa maandalizi chini ya miaka 20 mwaka 2023.(AFP).