LAGOS, Nigeria
WINGA wa kimataifa wa Nigeria, Henry Onyekuru, anaweza kurudi Galatasaray kwa mara ya tatu kwenye dirisha la uhamisho la Januari.Nyota huyo wa zamani anayemilikiwa na Everton anachukuliwa kuwa ziada ya mahitaji katika klabu ya ‘Ligue 1’ ya Monaco na hajapiga mpira kwenye mchezo rasmi na miamba hiyo kwa zaidi ya miezi mitatu.


Onyekuru hapo awali alifurahia mafanikio mawili ya mkopo huko Galatasaray, akifunga mabao 17 katika mechi 56 na kuwasaidia kushinda Ligi Kuu na Kombe la Uturuki mnamo 2019.Mwakilishi wa nyota huyo wa Super Eagles amethibitisha kuwa ‘Simba’ hao wanafikiria uwezekano wa kumsaini Mnigeria huyo na angependelea mkataba wa kudumu badala ya mpango mwengine wa mkopo wa muda mfupi.

“Kuna uvumi. Inakuja kwenye sikio langu. Galatasaray ni chaguo muhimu kwa Onyekuru. Uhamisho au mkopo, tutaona.,” Wakala wa Henry Onyekuru aliwaambia waandishi wa habari wa Uturuki.”Lakini natumai itakuwa kwa muda mrefu. Siwezi kusema chochote juu ya hali ya majadiliano na Monaco”.Klabu ya Falme za Kiarabu ya Al-Jazira FC pia inavutiwa na kumsaini Onyekuru ambaye yuko chini ya mkataba na Monaco hadi Juni 2024.(Goal).