BOSTON, Marekani
Mchezaji wa zamani wa Boston Celtics KC Jones ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 88
GWIJI wa zamani wa mpira wa kikapu aliyechezea timu ya Boston Celtics kwenye Ligi Kuu ya NBA ya Marekani, KC Jones, ameaga dunia.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya Boston Celtics, ilitangazwa kwamba KC Jones amefariki akiwa na umri wa miaka 88.

Jones ambaye alikuwa mchezaji nyota wa Boston Celtics na kuchangia mafanikio makubwa kwenye miaka ya 1960, aliwahi kuiongoza timu yake kubeba ubingwa wa NBA mara nane.
Jones, aliyekuwa mlinzi wa uhakika kwenye mpira wa kikapu, pia alishinda medali ya dhahabu na timu ya taifa ya Marekani kwenye Michezo ya Olimpiki ya Melbourne mwaka 1956.

Pia aliwahi kuifundisha Celtics kati ya mwaka 1983 na 1988, na kushinda ubingwa mara mbili kama kocha mkuu.Jezi ya nambari 25 ya Jones iliyotundikwa kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Wachezaji Maarufu, ilistaafishwa na Boston