LONDON, England
MSHAMBULIAJI yoso wa Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland ameweka wazi kuwa beki wa kati raia wa Senegal na Napoli ya Italia, Kalidou Koulibaly, ni moja kati ya mabeki bora zaidi duniani.

Haaland amesema beki huyo ana sifa za kipekee na amekua na umakini mkubwa wa kuwakaba washambuliaji hasa wenye makali, hivyo hana budi kuweka hadharani kwa kusema Koulibaly ni beki bora.

Mshambuliaji huyu alimtaja Koulibaly alipohojiwa na chombo cha habari cha Norway, ambacho kilimuhoji kuhusu changamoto alizowahi kukutana nazo uwanjani, na ndipo alipomtaja beki huyo.
Wachezaji wengine waliotajwa na Haaland kama mabeki bora duniani ni beki wa Real Madrid, Sergio Ramos pamoja na beki wa mabingwa wa England, Liverpool, Virgil van Dijk.

“Nadhani walinzi bora watatu duniani ni Sergio Ramos, Virgil van Dijk na Kalidou Koulibaly.
“Hawa wote watatu ni wana miili, lakini pia wana akili kwa namna wanavyocheza”, alisema, Erling Haaland.

Halaand alikutana na kazi ya Koulibaly wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2018/19 wakati akiwa na FC Salzburg.

Ubora wa Kolibaly ulifikia hatua ya kuzigonganisha klabu za Liverpool, Manchester City, PSG na Manchester United zilizokua na lengo la kumsajili, lakini, uongozi wa Napoli ulifanikiwa kumbakisha kwa kumsainisha mkataba mpya.(Goal).