BAGHDAD,IRAQ

MIJI kadhaa nchini Iraq inakabiliwa na kitisho cha kushuhudia upungufu mkubwa wa nishati ya umeme baada ya Iran kupunguza kiwango cha gesi inayosafirishwa kwenda nchini humo.

Wizara ya nishati ya nchi hiyo ilisema wiki mbili zilizopita kwamba, Iran ilipunguza mauzo yake ya gesi kwa Iraq hadi milimita za ujazo milioni tano kutoka milimita za ujazo milioni 50 kwa sababu ya kusuasua kwa malipo.

Pia serikali mjini Tehran iliiarifu serikali ya Iraq kuwa inalenga kupunguza zaidi kiwango cha usambazaji wa gesi hadi milimita za ujazo milioni tatu iwapo Baghdad itashindwa kulipa deni inalodaiwa.

Waziri wa nishati wa Iran Reza Ardakanian alipangiwa kufanya ziara mjini Baghdad kujadiliana na mwenzake wa Iraq namna nchi hiyo inaweza kulipa deni la huduma ya gesi kutoka Iran.