NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya soka ya Jadida juzi imetoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya New Version ikiwa ni muendelezo wa ligi daraja la pili Mkoa wa Kaskazini Pemba.

 Mchezo huo uliotimua vumbi majira ya saa 10:00 jioni  ulikuwa wa ushindani mkubwa.

Mabao ya Jadida yaliwekwa wavuni na Seif Mmaka dakika ya 24 na Nasir Nassor aliongeza bao la pili dakika ya 26 na kudumu hadi mapumziko.

 Kurudi uwanjani kumalizia kipindi cha pili timu hizo zilifanya mabadiliko.

Dakika ya 46 Hamza Ramadhan wa timu ya New Version alifunga bao la kufutia machozi,huku bao la tatu la timu ya Jadida likifungwa na Mohamed Issa Saburi dakika ya 73.