MPENZI msomaji wangu wa Zanizbar Leo, katika safu yetu hii ya tiba asilia leo nimewatayarishia namna ya kupunguza unene bila ya kufanya mazoezi.

Kama tunavyojua kuna watu wengi wamekuwa wakijiona kuwa wanene bila ya kukusudia jambo ambalo hakuna anaependa kufikia hali kama hiyo bila ya shaka.

Taizo hili si kwa Zanzibar au Tanzania kwa ujumla, Afrika bali ni tatizo la dunia watu kujiona kuwa wanene ghafla bila ya kutarajia.

Hivyo ukiona hali hiyo usikate tamaa ya kuupunguza mwili wako hasa kama huna muda wa kufanya mazoezi.

Kwa maana hiyo tiba nyepesi sana ya kupunguza mwili kwa njia ya asili ni pamoja na kutumia kotmiri, kitango, ndimu au limao pamoja na tangawizi.

Vitu vyako vyote hivi unavikata vidogo vidogo na baadae kuvisaga kwa kutumia blenda na baadae kuvichuja na kuwa tayari kwa matumizi yaani kunywa.

Baada ya kunywa tu basi ndani ya wiki mbili tu utakuwa tayari umejitibu tatizo la unene.

  • Chukua nanaa yako kifungu kimoja
  • Katakata kitango chako bila ya kumenya
  • Katakata tangawizi yako mbichi
  • Na mwisho unakatakata limao au ndimu
  • Gilasi moja ya maji safi ya kunywa

Baadae unachukua vitu vyako hivyo na kuvitia maji na kuvisaga na kuwa rojo zitozito.

Chuja kwa kutumia kichujio baadae unaweka kwenye gilasi na kuanza kunywa, basi ndani ya wiki mbili kama utafanya hivyo amini unene utaondoka bila ya kufanya mazoezi.