NA ZAINAB ATUPAE
LIGI daraja la pili Mkoa wa Kaskazini Pemba imeendelea kuchanja mbuga kwa kupigwa mchezo katika ya Junguni United na Super Star Micheweni.


Mchezo uliopigwa uwanja wa Junguni majira ya saa 10:00 jioni ambao ulikuwa wa ushindi,huku kila mmoja akisa ushindi kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo.


Katika mchezo huo timu ya Junguni United imetoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Super Star Micheweni.


Hadi timu zinakwenda kupata mapumziko mafupi hakuna iliofanikiwa kuzifumua nyavu za mwenzake.
Kurudi kumalizia kadika 45 za kipindi cha pili timu hizo ziliingia na kasi,huku kila mmoja ikiangalia vyavu za mwenzake.


Dakika ya 64 Ali Mohamed Khatib wa Super Star Micheweni alifanikiwa kuweka bao la kufuta machozi, mabao ya Junguni yalifungwa na Yahya Hussein dakika 60 na la pili lilimaliziwa na Azizi Salim dakika ya 81.