NAIROBI,KENYA

KWA mara nyengine Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amewaagiza wahudumu wa Afya kurejea kazini mara moja.

Akizungumza baada ya mkutano na waziri wa Leba Simon Chelugui na Baraza la Magavana kujadili mgomo unaoendelea, Kagwe alisema mgomo huo ni kinyume na sheria,kwani wahudumu hao walipuuza agizo la mahakama lililowataka warejee kazini.

Kagwe alisema inasikitisha kuona wahudumu wa afya wakigoma kipindi hiki cha korona huku wagonjwa wakiendelea kuhangaika.

Alisema serikali inaendelea kufanya kila iwezalo ikiwemo  kuwajiri wahudumu wengine ili wagonjwa wazidi kupata huduma.

Alisema masuala yote yaliyoibuliwa na wahudumu hao, yalishughulikiwa.

Alisema hadi sasa wameshirikiana na serikali za kaunti kuwapa vifaa vya kujikinga PPEs, Shughuli ya kuwapandisha vyeo inaendela na majadiliano yanaendelea kuhusu kubuniwa kwa Tume ya kitaifa ya Afya.

Kuhusu Bima na Mishahara Kagwe alisema inashughulikiwa.

Ikumbukwe kuwa madaktari walianza mgomo wao wa kitaifa hivyo kujiunga na wauguzi pamoja na maofisa wa kliniki wanaolalamika kwamba wamepuuzwa na serikali