NA MARYAM HASSAN

KESI iliyokuwa inamkabili mshitakiwa Mussa Simai Ali (23) mkaazi wa Jambiani, imeshindwa kusikilizwa kwa sababu mahakama aliyofikishwa mshitakiwa huyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Hayo yamebainika mara baada ya mshitakiwa huyo kufikishwa mbele ya Hakimu wa mahakama ya wilaya Mwera, Taki Abdalla Habibu.

Hakimu huyo alisema, mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, hivyo aliahirisha hadi Disemba 30 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa ushahidi.

Kwa mujibu wa maelezo ya hati ya mashitaka dhidi ya mshitakiwa huyo, inadaiwa kutenda kosa la kubaka tukio ambalo ametenda mnamo mwezi wa Machi mwaka huu siku na tarehe isiyojulikana majira ya saa 2:00 za usiku, huko Jambiani wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini Unguja.

Mshitakiwa huyo adaiwa kumuingilia kimwili mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 17 huku akijua kuwa kosa hilo ni kinyume na sheria.

Mara baada ya kusomewa shitaka hilo na Wakili wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Ayoub Nassor, aliiomba mahakama kuahirisha shauri hilo.

Vile vile mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa sababu Hakimu husika hayupo na kuamriwa kupelekwa rumande.