JUBA, SUDAN KUSINI

RAIS wa Sudan Kusini, Salva Kiir ameteua magavana sita watakongoza majimbo mbalimbali ya nchi hiyo.

Uteuzi huo umefanyika kufuatia mshauri wa usalama wa nchi hiyo Tutkew Gatluak kufanya mazungumzo ya muda mrefu na rais kuthibitisa uteuzi huo.

Miongoni mwa walioteuliwa ni pamoja na Mery Ludyra ambaye atakuwa msaidizi gavana wa jimbo la mshariki ya Eqauteria akitokea chama cha SPLM-IO.

Gavana mwengine ni Zacharia Joseph Garang, ambaye atakuwa msaidizi gavana wa jimbo la Western Bhar El Ghazal akitokea chama cha SPLM-IG.

Mwengine ni Tor Tungwar Kueiguong, msaidizi gavana katika jimbo la Unity akitokea chama cha SPLM-IO.

Mengine ni  Poth Madit, msaidisi gavana jimbo la Lakes kutoka chama cha  SPLM-IO na Badagbu Daniel , msaidizi gavana jimbo la  Western Eqauteria kutoka chama cha SPLM-IG na  Antifas Nuogk, msaidizi gavana jimbo la Jonglei.