NA VICTORIA GODFREY
Uongozi wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Mwanza (MRBA) umesema unatarajia kuendesha ligi ndefu ya Mkoa MRBA msimu ujao.
Kamishna wa Kamati ya Ufundi na Mashindano wa MRBA,Haidari Abdul,alisema lengo ni kutoa fursa kwa wachezaji kucheza michezo mingi wapate uzoefu.
Alisema kuwa itawasaidia kujijengea ujasiri wa kupambana na mikoa mingine na kuweza kupata matokeo mazuri.
” Mwaka huu tulishiriki ligi ya klabu, hivyo tulijifunza mengi na tukaona kuna haja msimu unaokuja tuandae ligi ndefu ili wachezaji wacheze michezo mingi ili kupata uzoefu ,” alisema Abdul.
Kamishna huyo alisema lengo ni kuonyesha ushindani na kushiriki kikamilifu kwenye ligi za kitaifa na kimataifa.