NA RAHMA JUMA

Mavungwa shehia ya Mbuzini kisiwani hapa, kimepata mafanikio baada ya kuongeza ubunifu wa bidhaaa za biashara.

Kikundi hicho kinachotumia mazao ya chakula ya asili na miti shamba kimefanikiwa kufanya ubunifu wa bidhaa zinazotibu maradhi mbali mbali ya binaadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari za ubunifu, Katibu wa kikundi hicho, Meiye Hamad Juma alisema bidhaa walizobuni ni pamoja na unga wa lishe unaotayarishwa kwa kutumia ndizi ya koroboi na kokwa za tango ambazo hutumiwa kwa lishe bora na kutibu vidonda vya tumbo, miguu, kujenga mifupa kwa watoto na kuondoa maradhi.

Alisema wanatengeneza dawa za ngozi pamoja scribe ambayo imepata sifa kubwa ndani na nje ya

kisiwa cha Pemba inayotayarishwa kwa miti shamba pamoja na zao la mwani.

Bidhaaa nyengine iliyobuniwa na kikundi hicho ni majani ya chai ambayo hutibu maradhi katika mwili wa binaadamu yanayotayarishwa kwa miti shamba isiyopungua tisa.

Wakati huo huo baadhi ya watumiaji wa bidhaa hizo waliozungumza na waandishi wa habari wakati

wakununua bidhaa hizo kwenye duka la kikundi hicho, walihakikisha ubora wa bidhaa hizo kwa afya ya binaadamu na kuwashauri wananchi wenye matatizo ya aina hiyo kufika kwenye soko hilo kujipatia bidhaa hizo.