NA ZAINAB ATUPAE
TIMU ya soka ya Kikwajuni SC leo inatarajia kucheza na timu ya Shangani kucheza mechi ya kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na ligi.


Kikwajuni ilishuka daraja msimu uliomalizika kutoka daraja la kwanza kanda ya Unguja na msimu huu itacheza daraja la pili Mkoa,huku Shangani ikishiriki daraja la pili wilaya ya mjini.


Akizungumza na gazeti hili katibu wa timu ya Shangani Abdalla Chagua,alisema mechi hiyo ni miongoni mwa maandalizi ya kujiandaa na ligi yao ambayo hadi muda huu hawajajua lini itaanza.


Alisema wamecheza mechi mbali mbali za kirafiki na timu za madaraja tofauti lengo ni kupata uzoefu.
Aidha aliwataka wachezaji kuendelea kuwa wastahamilivu huku wakisubiri taarifa kamili ya ligi hiyo.