PARIS,UFARANSA
MAELFU ya nyumba nchini Ufaransa na Uingereza zimeachwa bila umeme baada ya kimbunga Bella, kupiga baadhi ya maeneo na kusababisha mvua kubwa na upepo mkali.
Takribani nyumba elfu 34,000 za mashariki na katikati mwa Ufaransa ziLIkatiwa umeme,wakati kimbunga Bella kikiendelea kupiga katika maeneo mengine ya nchi.
Kimbunga Bella kilisababisha safari nyingi za ndege kutatizika nchini Ufaransa.
Uingereza nayo imekabiliwa na kimbunga Bella kilichosababisha nyumba kufunikwa na mafuriko katika baadhi ya maeneo ya Northamptonshire na Bedfordshire.
Katika eneo la kusini mwa England, zaidi ya watu 1,300 walishauriwa kuondoka kwenye makaazi yao wakati wa sikukuu ya Krismasi.
Wakati huohuo, nyumba takribani elfu 20,000 huko Wales nazo ziliachwa bila ya umeme na safari za treni kucheleweshwa kutokana na kadhia ya miti kuanguka katika njia za reli.