LONDON, England
MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp, ametupilia mbali uvumi kwamba mshambuliaji, Mohamed Salah, hana furaha klabuni hapo.Hivi karibuni Salah aliliambia gazeti la Hispania kwamba alikuwa amesikitishwa kutokuwa nahodha katika mechi dhidi ya FC Midtjylland wakati Trent-Alexander Arnold alipofanywa kuwa nahodha.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri mwenye umri wa miaka 28 pia alitolea nje kuhamia Real Madrid au Barcelona.
“Mo yuko katika hali nzuri, wakati mzuri na umbo zuri kabisa, hilo ndilo jambo muhimu zaidi kwangu”, alisema, Klopp.
“Hatukuwa na picha [kutoka uwanja wa mazoezi] asubuhi ya leo (jana), lakini, ikiwa tungekuwa nazo ungemuona akicheka sana.

“Zilizobakia ni nzuri kwako [chombo cha habari] kuandika, lakini, kwa ndani, hakuna kitu kweli”.Kufuatia kuchapishwa kwa mahojiano na Salah, alitoka benchi na kufunga mara mbili katika ushindi wa 7-0 wa ligi huko Crystal Palace. Ilimchukua jumla ya magoli 13 kileleni mwa ligi hiyo msimu huu na kusaidia kuhakikisha Liverpool ambayo inakaribisha West Brom kesho, inakuwa juu kwenye Krismasi kwa msimu wa tatu mfululizo.
Wekundu hao hawakufanikiwa kuendelea na kumaliza kileleni katika 2018-19 baada ya kulikosa kwa Manchester City, lakini, walishinda taji la 2019-2020.

“Ni wazi inamaanisha wewe sio bingwa wa moja kwa moja mwezi Mei wakati wewe ni kinara wa Krismasi,” alisema Klopp. “Vyenginevyo tungekuwa tumeshinda mara mbili tayari.”Ni nafasi nzuri zaidi ambayo unaweza kuwa nayo kwa sasa, lakini, hiyo ndiyo yote. Hata hatujacheza nusu ya msimu. Ni nzuri, hakuna kitu chengine chochote.
“Miaka miwili iliyopita, wakati hatukushinda ligi baada ya kuwa juu wakati wa Krismasi, haikuwa juu ya ukosefu wa umakini. Ilikuwa ubora wa wapinzani na ubora huu bado uko nje hapo.”